Ushirika Wa Wakristo Wa Kukomboa Nyakati.

Karibuni kwenye Ushirika wa Wakristo wa Kukomboa Nyakati. Hili ni Tawi la kanisa la Mkusanyiko wa Watu kwenye Mlima wa Ishara ya Mungu. Hili ni kanisa ambalo linajumuisha huduma ya kimishonari na watu wa matabaka mbalimbali.

Ushirika wa Wakristo wa Kukomboa Nyakati ni Tawi la kanisa la Mkusanyiko wa watu kwenye mlima wa Ishara ya Mungu na washirika wake hutumia lugha ya Kiswahili kwa mawasiliano. Mchungaji wa ushirika huu ni Pasta Daniel Kitheka. Yeye ameoa mpenzi wake Veronica Kitheka na wamebarikiwa na watoto watatu, Emmanuel, Emma na Joy.

Lengo letu ni kukomboa wakati na kufikishia watu nuru ya Mungu ili wabadilike, wageuze nia na wapate nguvu za kiroho. Tutembeleeni mpate kushuhudia sababu inayofanya Mlima wa Ishara ya Mungu kuwa tofauti na huduma zingine.

Idara za Huduma
Huduma ya watoto
Huduma ya vijana
Huduma ya kina Baba
Huduma ya kina Mama
Huduma ya Jamii

Masaa ya Ibada
Ibada kuu Jumapili – 10:30 am
Ibada ya watoto Jumapili – 10:30 am
Moambi Alhamisi -7:00 pm
Ushirika Ijumaa – 7:00 pm (Mji wa Rialto)